1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uhalifu

Marekani yazuwia utekaji wa meli katika bahari ya Ghuba

27 Novemba 2023

Jeshi la majini la Marekani limewakamata watu watano walioshambulia meli y amizigo katika ghuba ya Aden, limesema jeshi la Marekani Jumatatu, na kuongeza kuwa meli hiyo na wanafanyakazi wake wako salama.

https://p.dw.com/p/4ZU5r
Meli ya "Central Park"
Marekani yasema jeshi lake la maji limezuwia utekaji wa meli hili ya ya Central Park, katika Ghuba ya Aden.Picha: Zodiac Maritime/AP/picture alliance

Maafisa wa Marekani wameripoti kwamba meli ya mizigo iliyotuma ujumbe wa dharura ikiwa kwenye bahari ya ghuba ya Aden baada ya kutekwa na watu waliokuwa na silaha iko salama, baada ya meli ya kivita ya jeshi la Marekani kuingilia kati.

Katika taarifa yake jeshi la Marekani limesema meli yake ya USS Mason kwa msaada wa meli za washirika wake, iliiwalazimisha washambuliaji kuiachilia  Meli hiyo iliyotambuliwa kwa jina la Central Park, iliyokuwa imebeba mzigo wa kemikali.

Soma pia: Uharamia uliochacha katika pwani ya Somalia unazidi kuzusha hofu miongoni mwa makampuni yanayosafiri kupitia eneo hilo.

Washambuliaji watano waliojaribu kukimbia kwa kutumia boti ya mwendo kasi walisalimu amri baada ya kukimbizwa na meli ya kivita ya Marekani.Taarifa ya jeshi la Marekani pia ilisema makombora yalifyetuliwa kutoka maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa Kihouthi nchini Yemen kuelekea meli yao na ile ya mizigo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW