1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Mashambulizi ya droni ya Uturuki yawaua raia 27 nchini Syria

Angela Mdungu
25 Oktoba 2024

Mashambulizi ya droni ya Uturuki yamewaua raia 27 nchini Syria ndani ya saa 24 zilizopita, kufuatia shambulizi kubwa dhidi ya kampuni ya ulinzi karibu na Ankara.

https://p.dw.com/p/4mDbh
Waombolezaji Uturuki
Wanafamilia na jamaa wakiomboleza baada ya shambulio la bomu kwenye jengo la serikali la "Turkish Aerospace Industries" (TAI), mjini Ankara Oktoba 24, 2024. Picha: Adem Altan/AFP

Hayo yameelezwa na Shirika la uangalizi wa haki za binadamu la Syria ambalo limeeleza kuwa, vikosi vya Uturuki vimezidisha kwa kiasi kikubwa mashambulizi yake ya angani na ardhini kaskazini na mashariki mwa Syria tangu jana Alhamisi. Shirika hilo limerekodi jumla ya mashambulizi 45 ya Dronina manne ya ndege za kivita yaliyoilenga miundombinu ya maji, umeme na vituo vya gesi. Uturuki ilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi nchini Iraq na Syria Jumatano wiki hii, ikiwashutumu kwa shambulizi lililowaua watu watano katika kampuni ya ulinzi karibu na mji mkuu wa Ankara.