Mashambulizi ya Israel yawauwa watu 12 Gaza
18 Desemba 2024Matangazo
Msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal ameliambia shirika la habari la AFP kuwa Wapalestina 10 wameuawa kufuatia shambulio la Israel lililolenga nyumba moja katika eneo la Beit Lahia.
Bassal ameongeza kuwa mtoto mmoja ameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio lingine tofauti lililolenga nyumba karibu na eneo la Jabalia, sehemu ambayo vikosi vya Israel vimeelekeza oparesheni zao katika miezi ya hivi karibuni.
Zaidi ya miezi 14 tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas, Marekani imeeleza matumaini kuhusu uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano ukanda wa Gaza.