Watu watano wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi mawili mkoani Mubanza magharibi mwa Burundi. Mjini Bujumbura ifikapo saa 12 jioni idadi kubwa ya askari wa usalama hutawanya mitaani kupiga doria. Pamoja na hayo Waziri wa usalama Alain Guillaume Bunyoni amesema kwa jumla hali ni ya kuridhisha.