1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIraq

Mashambulizi ya Uturuki Kurdistan yaikasirisha Iraq

8 Aprili 2023

Rais wa Iraq Abdel Latif Rashid leo amelaani shambulizi la Uturuki dhidi ya uwanja wa ndege wa Sulaimaniyah uliopo kwenye mkoa wa Kurdistan eneo ambalo ni kitovu cha mvutano kati ya mataifa hayo mawili.

https://p.dw.com/p/4PptI
Eneo la nje la Uwanja wa Ndege wa Suleimaniyah
Uwanja wa Ndege wa Suleimaniyah huko KurdistanPicha: SHWAN MOHAMMED/AFP/Getty Images

Kiongozi huyo amesema kitendo cha kuushambulia uwanja wa ndege kwa mabomu hakina msingi wowote wa kisheria na ameitaka serikali mjni Ankara kuomba radhi na kusitisha hujuma zake ndani ya ardhi ya Iraq.

Amesema Uturuki ni lazima ikomeshe kile amekitaja kuwa "matendo ya kichokozi" kaskazini mwa Iraq inakoendesha operesheni ya kijeshi ya muda mrefu inayoilenga jamii ya Wakurdi kwenye mkoa wa Kurdistan unaojitawala wenyewe.

Serikali ya Ankara inadai eneo la Sulaimaniyah limegeuka hifadhi ya wafuasi wa chama cha kikurdi cha PKK kilichopigwa marufuku nchini Uturuki.