Mashirika ya misaada yahofia athari za vurugu Kongo
9 Februari 2024Mapigano kati ya waasi wa kundi la M23 na vikosi vinavyoiunga mkono serikali ya Kongo, ambayo yameendelea kwa zaidi ya miaka miwili, yamezidi hasa katika mkoa wa Kivu Kaskazini, ambako raia wanakabiliwa na mashambulio ya mabomu, maelfu wakilaazimika kukimbia na watoto kupotea.
Soma zaidi: Jeshi la DR Kongo lawazuiwa waasi wa M23 kuutwaa mji wa Sake
Jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa nchini Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo limesema katika taarifa kwamba ongezeko la waathirika wa kiraia na matumizi ya silaha nzito katika maeneo ya raia, ikiwemo kambi za wakimbizi linatia wasiwasi.
Soma zaidi: Wanne wauawa, 25 wajeruhiwa kwa mabomu ya M23
Mapigano hayo yamesababisha uhamaji mkubwa kuelekea maeneo kadhaa, na kuchochea hatari ya wale waliolazimika kukimbia na jamii za wenyeji wao.
Soma zaidi: Jeshi la DRC lapambana na M23 Kivu Kaskazini
Jukwaa hilo ambalo linawakilishi zaidi ya mashirika 120 ya kimataifa yanayoendesha shughuli zake Kongo, limetaka hatua za haraka kuwalinda raia na kuhakikisha uwepo wa njia za kiutu.