Maandamano ya Msumbiji yaathiri masoko ya ndani na nje
14 Desemba 2024Halli hiyo inadhihirika ikiwa ni takribani miezi miwili ya machafuko ya baada ya uchaguzi am,bay mara kwa mara huzuia uagizaji bidhaa kutoka Afrika Kusini. Maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Msumbiji ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 100, kulingana na mashirika ya kiraia yamesababisha ugumu wa kuingia katika maeneo ya katikati ya jiji. Kadhalika yametatizoa safari katika mpaka mkuu na Afrika Kusini, njia muhimu ya uagizaji bidhaa ambapo katika majuma yaliopita ufungwa mara kwa mara hali inayo tatizo mwenendo wa hali ya uchumi kwa nchi zote mbili. Viazi, karoti, vitunguu na mazao mengine yanayoletwa kutoka Afrika Kusini ni vigumu kupatikana sokoni. Kiongozi mkuu wa upinzani Venancio Mondlane Jumatatu anatazamiwa kutangaza wimbi jipya la maandamano.