1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa kuzuia usafirishaji wa tembo mijini na kwenye 'zoo'

28 Agosti 2019

Katika mkutano uliofanyika Geneva Uswizi, Wataalam wa wanyama pori wamesema uamuzi wa kupinga ndovu kutouzwa katika maeneo ya mijini ya kuwahifadhi wanyama pori, yaani zoo ni ushindi mkubwa kwa ndovu.

https://p.dw.com/p/3OdUU
Sambia Elefant im Chobe Nationalpark
Picha: picture-alliance/S. Reboredo

Nchi zilizo kwenye mkataba wa kimataifa juu ya hatari ya kutoweka kwa aina mbalimbali za mimea na wanyama zimekubaliana kupunguza uuzaji wa tembo waliokamatwa nchini Zimbabwe na Botswana hatua ambayo imewafurahisha walinzi wa mazingira na kuyavunja moyo baadhi ya mataifa  ya afrika yanayohusika. 

Katika mkutano uliofanyika Geneva Uswizi, Wataalam wa wanyama pori wamesema uamuzi wa kupinga ndovu kutouzwa katika  maeneo ya  mijini ya kuwahifadhi wanyama pori , yaani zoo ni ushindi mkubwa kwa ndovu.

Jumuiya ya ulaya imependekeza maelewano ambayo yanazuia usafirishaji wa ndovu hai nje ya Afrika isipokua katika mazingira ambayo watalazimika.

"Washiriki wengi kwa CITES waliamua kwamba ndovu wa Kiafrika ni wa Afrika. Ndio, bado kuna mipango kadhaa, bado kuna vifungu vya mkutano ambavyo vinaweza kuruhusu ndovu wengine wa Kiafrika kusafirishwa kwa katika hifadhi za kitaalamu za kuongeza  idadi ya vizazi  `ex-situ`. Lakini msingi ni kwamba, siku za kuuza nje tembo wa Kiafrika kwa mzabuni mkubwa zaidi, au katika mbuga za wanyama Merekani au hata kwa Umoja wa Ulaya, na kadhalika.Siku hizo zimekwisha." Amesema D.J Schubert ambaye ni mtaalam katika taasisi ya ustawi wa wanyama pori  

Azimio jipya linalenga kusitisha kusafirisha tembo wa Kiafrika waliokamatwa na kupelekwa Marekani, Uchina na nchi nyengine ambazo sio makazi asilia ya tembo.
Azimio jipya linalenga kusitisha kusafirisha tembo wa Kiafrika waliokamatwa na kupelekwa Marekani, Uchina na nchi nyengine ambazo sio makazi asilia ya tembo.Picha: AP

Walinzi wa mazingira walielezea mabadiliko hayo kwa kutoa mfano, wakisema ingeruhusu tembo ambaye yupo Ufaransa kusafirishwa kwenda karibu na Ujerumani bila kulazimika kurudishwa barani Afrika kwanza.

Lakini azimio jipya linalenga kusitisha kusafirisha tembo wa Kiafrika waliokamatwa na kupelekwa Marekani, Uchina na nchi nyengine ambazo sio makazi asilia ya tembo. Azimio hilo limeungwa mkono na kupitishwa  kwa jumla ya kura ya 87, huku kura 29 zikipinga hatua hiyo.

Mkurugenzi wa wanyama pori wa Humane Society International, Audey Delsink amepongeza hatua hio ingawa anahisi uamuzi huo haukuweka vikwazo vya kutosha katika marufuku ya biashara ya ndovu hai.

Takwimu zinaashiria kuwa Botwana na Zimbwabwe zinaongoza kwa idadi ya wingi wa ndovu wa kiafrika duniani zikiwa na jumla ya ndovu 200,000.

Takwimu zinaashiria kuwa Botwana na Zimbwabwe zinaongoza kwa idadi ya wingi wa ndovu wa kiafrika duniani zikiwa na jumla ya ndovu 200,000
Takwimu zinaashiria kuwa Botwana na Zimbwabwe zinaongoza kwa idadi ya wingi wa ndovu wa kiafrika duniani zikiwa na jumla ya ndovu 200,000Picha: Getty Images/AFP/M. Bhuiyan

Baadhi ya viongozi wa kiafrika katika mkutano huo wamesema uamuzi utaathiri pakubwa viwango vya mapato na wangetaka kuruhusiwa kufanya watakavyo na ndovu wao. Manesushe Munodawafa ambaye ni katibu mkuu wa wizara ya mazingira Zimbwabwe amesema:

"Zimbabwe ina tembo elfu 84. Tuna uwezo wa kuwa na tembo elfu 54. Kwa hivyo, tuna tembo zaidi ya 30,000 kuliko ikolojia yetu inavyoweza kuhimili. Na athari ya hii ni kwamba sasa tunapaswa kubeba mzigo huo, na tunapaswa kubeba gharama, ambayo hakuna mtu mwingine ulimwenguni anashiriki nasi. "

Wakati huo huo Audrey Delsink amesema kukamatwa kwa ndovu wa kiafrika kwa lengo la kuwasafirisha katika mbuga za wanyama na maeneo mengine kunaathiri utangamano wa wanyama hao katika makundi yao ya kijamii.

Mwandishi:Saumu Njama/APE