1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya ASEAN yaunda rasmi jumuiya

22 Novemba 2015

Mataifa ya kusini mashariki mwa Asia leo Jumapili(22.11.2015) yameaunda rasmi jumuiya ambayo itajaribu kujenga uhamishaji huru wa biashara na mitaji katika eneo hilo lenye jumla ya wakaazi milioni 625.

https://p.dw.com/p/1HACF
Malaysia ASEAN Gipfel
Viongozi wa jumuiya ya ASEAN mjini Kuala LumpurPicha: picture-alliance/dpa/R. Yongrit

Eneo hilo lina uwezo wa uchumi jumla unaofikia dola bilioni 2.6.

Tangazo la Jumuiya hiyo lilitiwa saini na viongozi wa mataifa 10 wanachama wa jumuiya ya mataifa ya kusini mashariki mwa Asia mjini Kuala Lumpur, mji ambao mwaka huu umekuwa mwenyeji wa mkutano huo wa kila mwaka.

Jumuiya ya ASIEN inajumuisha mtazamo wa masuala ya kisiasa, usalama na utamaduni wa kijamii katika kanda ambayo ina serikali kuanzia ya kikomunisti nchini Vietnam na ya mchanganyiko baina ya raia na wanajeshi nchini Myanmar hadi serikali ya kifalme nchini Brunei pamona na nchi ya kidemokrasia ya Ufilipino.

Malaysia ASEAN Gipfel in Kuala Lumpur
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Ufilipino(kushoto) na mwenzake wa LaosPicha: AFP/Getty Images/M. Rasfan

Fursa zinazopatikana

Lakini ni jumuiya hiyo ya kiuchumi ambayo inatoa kwa nchi hizo fursa halisi kwa ajili ya ujumuisho katika kanda hiyo ambayo pato lake jumla (GDP) italifanya eneo hilo la dunia kuwa katika nafasi ya saba kwa uchumi mkubwa duniani.

Miaka 13 baada ya kuasisiwa kwa wazo hilo, viongozi hao hatimaye wametimiza ndoto yao ya umoja wa kiuchumi, wakiwa na matumaini ya kushindana na China na India.

Jumuiya hiyo ambayo inatambulika kwa kifupi kama AEC, tayari inafanyakazi na mingi ya misingi yake imetumika katika kanda hiyo kama kuondoa vikwazo vya ushuru wa forodha pamoja na vizuwizi vya viza miongoni mwa mambo mengine. Pia hatua hiyo imesababisha ushirikiano mkubwa zaidi ya kisiasa na kitamaduni.

Mataifa hayo yanalenga kuweka pamoja mikakati yao ya kiuchumi, kutambua uwezo wa utendaji wa kitaalamu wa kila nchi, na kushauriana kwa karibu zaidi kuhusiana na uchumi wa biashara ndogo ndogo pamoja na sera za kifedha.

Malaysia ASEAN Gipfel Barack Obama
Rais Barack Obama wa Marekani katika mkutano huo wa ASEANPicha: picture-alliance/dpa/W. Woon

Kuunganisha miundo mbinu

Pia wamekubaliana kuimarisha uwezo wao wa kuunganisha miundo mbinu kwa ajili ya usafirishaji na mawasiliano, kufanya bora zaidi miamala ya kielekroniki , kuleta mahusiano ya karibu ya viwanda ili kuruhusu matumizi ya nguvu kazi katika kanda hiyo, na kuimarisha uhusikani wa sekta ya binafsi katika uchumi.

Makundi manane ya wataalamu yataweza kufanyakazi kiurahisi katika kanda hiyo, ikiwa ni pamoja na wahandisi, wasanifu majengo, wauguzi , madaktari, waganga wa meno, wahasibu, wakaguzi ardhi na wataalamu wa masuala ya utalii.

Baada ya sherehe za utiaji saini, viongozi wa ASEAN walikutana na viongozi wengine wanane kutoka Asia na Pacific kwa ajili ya mkutano wa kila mwaka wa Mashariki mwa Asia, ikiwa ni pamoja na Marekani, China , Japan , Korea kusini, India, Urusi , Australia na New Zealand.

ASEAN Gipfel in Myanmar Li Keqiang 13.11.2014
Waziri mkuu wa China Li Keqiang katika mkutano wa ASEANPicha: Aung Thu/AFP/Getty Images

Rais wa Marekani Barack Obama alitarajiwa kuonesha wasi wasi wake katika mkutano huo leo juu ya kujitutumua kwa China katika bahari ya kusini mwa China.

Jana Jumamosi (21.11.2015) katika mkutano na viongozi wa ASEAN Obama alisema nchi zinapaswa kuacha kufanya madai yao kwa kutumia jeshi katika mzozo wa bahari ya China.

Mwandishi: Sekione Kitojo /rtre / dpae

Mhariri: Isaac Gamba