1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSamoa

Viongozi wa nchini za Jumuiya ya Madola wakutana Samoa

24 Oktoba 2024

Viongozi wa nchini wanachama wa Jumuiya ya Madola wanakutana hii leo katika kisiwa cha Samoa, huku ajenda kuu zikitarajiwa kujikita katika mabadiliko ya tabianchi.

https://p.dw.com/p/4mA1W
Mwanamfalme Charles
Mwanamfalme Charles akifungua mkutano wa kilele wa CHOGM mjini Kigali, Rwanda. Juni 24, 2022Picha: Chris Jackson/Getty Images

Viongozi na maafisa kutoka nchi 56 yenye historia na Ufalme wa Uingereza yanahudhuria mkutano huo wa Wakuu wa Serikali za Jumuiya ya Madola (CHOGM) ulioanza siku ya Jumatatu katika kisiwa hicho cha Samoa.

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer alisema siku ya Jumatatu kwamba Uingereza haitalileta suala la fidia kwenye mkutano huo wa kilele, lakini iko tayari kukutana na viongozi wanaotaka kulijadili.

Karibu Waafrika milioni 12.5 walisafirishwa kwa nguvu kwa meli na kuuzwa utumwani kati ya karne ya 15 hadi 19. Manusura wa safari hiyo ngumu walipelekwa kulima mashamba Barani Amerika.