Iran yashtumiwa kwa uzalishaji wa madini ya Urani
29 Desemba 2023Katika taarifa ya pamoja, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Marekani zimesema ''zinalaani hatua hiyo ambayo inazidisha mpango wa nyuklia wa Iran''.
Soma pia:Iran kurutubisha madini ya Uranium kwa asilimia 20
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa ''matukio hayo ni hatua katika mwelekeo mbaya kwa upande wa Iran na kwamba maamuzi hayo yanaonesha kutokuwepo kwa dhamira kwa upande wa Iran kushiriki katika kupunguza uzalishaji huo kwa nia njema na kusababisha tabia ya kutowajibika katika mazingira ya mivutano ya kikanda.
Soma pia: Iran kurutubisha urani na kukiuka makubaliano ya nyuklia
Akijibu ripoti hiyo ya IAEA, mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran Mohammad Eslami, amesema hakuna chochote kipya walichokifanya na shughuli zao zinafuata kanuni zilizopo.