1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matangazo ya BBC na VOA yamezimwa Burundi

7 Mei 2018

Matangazo ya Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC na ya Sauti ya Amerika, VOA hayasikiki nchini Burundi kuanzia leo, kufuatia uamuzi wa Baraza la Habari la Burundi kuifunga minara ya vituo hivyo.

https://p.dw.com/p/2xI63

Baraza hilo limesema sababu ya uamuzi huo ni ukiukaji wa sheria, kwa kurusha vipindi vyenye kauli za uchochezi na chuki. Hata hivyo, wapinzani wanasema hatua hiyo ni kunyamazisha sauti ya upinzani kuelekea kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba ambayo itapigwa nchini humo baadaye mwezi huu, ikipigiwa debe na serikali. Zaidi sikiliza mahojiano ya Daniel Gakuba na mwenyekiti wa Baraza la Habari la Burundi Karenga Ramadhani, ambaye ameanza kwa kuelezea sababu ya wao kuvifungia vituo hivyo.