Matarajio ya wanasiasa wa Ulaya katika uchaguzi wa Marekani
7 Novemba 2016Hebu fikiria , kwamba uchaguzi unafanyika nchini Marekani kesho Jumanne (08.11.2016) na kisha Trump ameshinda. Bara la Ulaya linahofu kubwa na fikira hiyo. Hillary Clinton kinyume chake anaonekana kueleweka zaidi katika uhusiano kati ya maeneo haya mawili yanayotenganishwa na bahari ya Atlantic. Ni nani kwa mtazamo wa watu wa Ulaya anafaa kushinda uchaguzi huu.
Kuna jengo moja peke yake katika bara la Ulaya kijiongrafia , ambalo lina jina la Donald Trump. Jengo hilo liko mjini Istanbul nchini Uturuki. Lakini tangu mwaka 2015 , wakati mgombea wa kiti cha urais nchini Marekani aliposema anapinga Waislamu kuhamia nchini Marekani , wanasiasa wa Uturuki pia wanataka kufuta jina la Trump katika jengo hilo.
Pamoja na hayo kundi la makampuni ya Trump limejenga viwanja kadhaa vya mchezo wa golf katika bara la Ulaya. Na hilo ndio jambo pekee linaloleta uhusiano kati ya Donald Trump na Ulaya.
Na tangu Donald Trump alipofanya ziara nchini Scotland mwezi Juni mwaka huu si jambo la kudai, lakini aliiteka na kuwafanya watu wavutike upande wake. Na ndivyo alivyofanya hadi kuteuliwa kuwa mgombea katika uchaguzi wa Marekani.
Mbunge wa Ujerumani katika bunge la Ulaya , David MacAllister ambaye naye binafsi ana asili ya Scotland , amemueleza mgombea huyo wa chama cha Republican kama hivi: "Donald Trump hatambuliki sana kwetu sisi watu wa Ulaya. Hatufahamu mengi kumhusu yeye. Hatufahamu mengi kuhusiana na sera zake za mambo ya kigeni, kwa kuwa hazungumzi mengi kuhusu hilo.
Na iwapo utaingia kwa undani zaidi , inaleta kidogo hofu. MacAllister ni mwenyekiti wa kundi la bunge la Ulaya , ambalo linashughulika na masuala ya uhusiano kati ya Ulaya na Marekani.
Ni wazi kwamba tunamfahamu Hillary Clinton vizuri zaidi hapa Ulaya. Anaamini kuhusu uhusiano imara kati ya Ulaya na Marekani. Pamoja nae tunahakika ya kufanikisha mambo mengi. Kwa kuwa waziri wa zamani wa mambo ya kigeni Hillary Clinton amekutana na wanasiasa wengi wa Ulaya waliopo hivi sasa.
Uhusiano na Ulaya
Kwa hiyo mtu anatarajia hali ya muendelezo wa mambo. Hadi sasa maraisi wengi kutoka chama cha Democratic na Republican waliendeleza hali ya uimara wa jumuiya ya NATO. Lakini Donald Trump tayari ameitikisa jumuiya hiyo ya ulinzi katika mataifa hayo ya Atlantic. Anataka tu kuendelea na jumuiya hiyo pale Ujerumani itakapolipia usalama wake.
David McAllister anajaribu kuyaeleza matarajio yake kwa njia ya kidiplomasia. Marekani na Umoja wa Ulaya wana uhusiano wa karibu sana . Tunapaswa kuweka mtazamo wetu katika kuimarisha hali hii, bila kujali matokeo ya uchaguzi. Tunapaswa kujitayarisha kwa hali mbaya ama nzuri.
Kuna wapenzi wa Trump lakini hata katika makao makuu ya Umoja wa Ulaya, hususan wanasiasa wa mrengo wa kulia. Mbunge wa Uingereza katika bunge la Ulaya Nigel Farage alishiriki katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi ya Donald Trump. Kutokana na ukosoaji mwingi dhidi ya Trump kuhusu matamshi yake na vitendo vya kuwadhalilisha wanawake , Farage alisema wakati alipohojiwa na kituo cha televisheni cha Fox nchini Marekani kwamba , Donald Trump ni binadamu, na kila binadamu ana doa lake, ambalo kwa Trump tunalijua lakini hatujui lolote la siri kwa upande wa Clinton hadi sasa. Ameongeza kwamba anachaguliwa rais wa Marekani na sio baba mtakatifu.
Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schaeuble alisema katika mkutano mjini Luxemburg alishangazwa sana alipomsikia Trump katika mdahalo katika televisheni akimtishia Clinton kwamba atamkamata akichaguliwa kuwa rais.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amemuita Donald Trump kuwa ni mhubiri wa chuki.
Mwandishi: Bernd Riegert / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Yusuf , Saumu