1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Matayarisho ya kuiokoa meli iliyotekwa nyara Somalia yaanza

18 Machi 2024

Polisi wa Puntland na wanamaji wa kimataifa wajiandaa kwa operesheni ya kuiokoa meli iliyotekwa nyara.

https://p.dw.com/p/4drxZ
Meli hiyo ya MV Abdullah ilitekwa nyara nje ya pwani ya Somalia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Meli hiyo ya MV Abdullah ilitekwa nyara nje ya pwani ya Somalia mwishoni mwa wiki iliyopita.Picha: SpokespersonNavy via X via REUTERS

Jeshi la polisi katika mkoa wa Puntland wenye mamlaka yake ya ndani nchini Somalia na jeshi la wanamaji la kimataifa wanajiandaa kufanya operesheni ya kuiokoa meli ya kibiashara iliyotekwa nyara na maharamia wiki iliyopita.

Meli hiyo ya MV Abdullah ilitekwa nyara nje ya pwani ya Somalia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Maharamia wa Kisomali ambao walikuwa wametulia kwa takriban muongo mmoja bila ya kufanya utekaji nyara wa meli za biashara.

Hatua hiyo imetangazwa siku mbili baada ya kikosi cha wanamaji cha India kuiokoa meli nyingine ya mizigo mnamo siku ya Jumamosi iliyokuwa inashikiliwa na maharamia.

Meli hiyo MV Ruen, iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Malta, ilitekwa nyara mwezi Desemba mwaka uliopita. Kikosi cha wanamaji cha India kilifanikiwa kuwakomboa wafanyakazi 17 wa meli hiyo na maharamia 35 walikamatwa.