MigogoroIsrael
Mateka 10 zaidi wa Israel waachiwa huru
29 Novemba 2023Matangazo
Shirika la Msalabaa Mwekundu limethibitisha kupokea kundi hilo la mateka na kuwakabidhi kwa mamlaka za Israel. Miongoni mwao ni wanawake 9 na msichana mmoja mwenye umri wa miaka 17.
Kwa upande wake Israel nayo imewaachia huru wafungwa 30 wa Kipalestina waliokuwa wakishikiliwa kwenye moja ya jela zake.
Israel na kundi la Hamas walikubaliana kurefusha muda wa kusitisha mapigano kwa siku mbili zaidi kuanzia jana baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya siku nne.
Tangu usitishaji mapigano ulipoanza Ijumaa iliyopita, kundi la Hamas limewaachia huru jumla ya mateka 81, wengi wakiwa raia wa Israel na mamlaka za Israel zimewatoa jela Wapalestina 180.