Matumaini mapya ya mazungumzo Sudan
29 Aprili 2023Hatua hiyo imeleta matumaini japo kidogo hata wakati mapambano yakiendelea. Perthes amesema pande hizo mbili hasimu ziliteua wawakilishi kwa ajili ya mazungumzo yaliyopendekezwa kufanyika Jeddah nchini Saudi Arabia au Juba, huko Sudan Kusini.
Hata hivyo ameongeza kuwa, swali kubwa ni iwapo wawakilishi hao watafanikiwa kufika na kukaa kwenye moja ya mazungumzo. Mjumbe huyo maalumu wa Umoja wa Mataifa hajaainisha ikiwa kuna muda maalumu uliotengwa kwa ajili ya mazungumzo hayo.
Soma zaidi:Milio ya risasi inaendelea kusikika nchini Sudan licha ya kauli ya kusitisha mapigano
Matarajio ya mazungumzo kati ya viongozi wa pande zinazotofautiana hadi sasa yamekuwa madogo. Ijumaa, kiongozi wa jeshi rasmi la serikali, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan katika mahojiano alisema kamwe hatokaa chini na kiongozi wa wanajeshi wa kikosi maalumu cha RSF Mohamed Hamdan Dagalo.
Kwa upande wake Dagalo alieleza kuwa atakuwa tayari kuzungumza ikiwa jeshi litasitisha uhasama. Mamia ya watu wameuwawa tangu Aprili 15 kutokana na mzozo wa kuwania madaraka kati ya pande hizo mbili
Soma zaidi:Sudan: Makubaliano ya usitishwaji mapigano kufikia tamati
Perthes alieleza kuwa aliliambia baraza la usalama kuwa pande zote mbili zilizo kwenye mzozo zilidhani zitashinda, alisema pia hata hivyo mitazamo yao imeanza kubadilika. Alisema, "Wote wanadhani watashinda, lakini kwa kiasi Fulani wanatoa nafasi ya kufanyika kwa majadiliano, awali neno majadiliano au mazungumzo halikuwa na nafasi”
Aliendelea kueleza kuwa, "Wakati tayari pande hizo zikiwa zimeshatoa kauli kuwa upande wa pili ni sharti ujisalimishe au uchague kufa, sasa wanasema pia kuwa wanakubali walau kufikiria kuwa na mazungumzo”.
Mapigano yanaendelea licha ya matumaini ya majadiliano
Pamoja na hayo, jeshi rasmi limekuwa likifanya mashambulizi ya anga kila siku na limesema limeendelea kudhibiti maeneo muhimu. Wakaazi wameeleza kwamba kwa upande wao RSF wameendelea kuuwa na nguvu zaidi katika mapambano ya ardhini mjini Khartoum
Mapigano hayo yanayoendelea, yamesababisha uharibifu wa miundombinu ya umeme, maji na mawasiliano huku matukio ya uporaji yakiharibu makazi ya wat una biashara. Maelfu ya raia wamekimbilia kwenye miji mingine na hata katika nchi Jirani