Matumaini ya kusitishwa mapigano Gaza yaongezeka
20 Desemba 2023Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema, mkuu wa shirika la ujajusi la nchi hiyo, anaongoza juhudi za kupatikana mkataba wa kusitisha vita na kundi la Hamas kwa ahadi ya kubadilishana mateka 129 wa Kiisraeli.
Soma pia: Kiongozi wa Hamas awasili Misri kwa mazunguzmo ya kusitisha mapigano Gaza
Duru zinasema kiongozi huyo wa shirika la Mossad, David Barnea, alikuwa na mkutano nchini Poland mapema wiki hii pamoja na Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, na Waziri Mkuu wa Qatar, Mohammed bin Abdulrahman Al Thani.
Soma pia: Wapalestina 19,400 wameuawa hii ikiwa ni kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza
Hayo yameripotiwa wakati kiongozi wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh, yuko mjini Cairo tangu mapema leo mchana kushiriki mazungumzo ya kusitisha mapigano huko Gaza. Analenga kutafuta mkataba utakaowezesha kupelekwa msaada zaidi wa kiutu ndani ya Ukanda wa Gaza na kuachiwa huru wafungwa wa Kipalestina.