1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauaji yaendelea Syria

11 Juni 2011

Kumekuwa na taarifa kwamba vikosi vya usalama vya Syria vimewaua kiasi waandamanji 25 wanaoipinga serikali, wakiwemo 11 katika eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/11Ybt
Rais wa Syria Bashar al-AssadPicha: picture-alliance/dpa

Vifo hivyo vipya vimetokea wakati wanajeshi wameanzisha operesheni ya matumizi ya nguvu ya kuzima upinzani katika mji wenye machafuko karibu na mpaka wa Uturuki.

Jana, waandamanaji walimiminika kwenye mitaa ya miji ya nchi hiyo baada ya sala ya Ijumaa, wengi wakitowa matamshi ya kejeli dhidi ya Rais Bashar al-Assad.

Türkei Ministerpräsident Recep Tayyip Erdogan in Ankara
Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip ErdoganPicha: dapd

Wakati huo huo, katika kile kinachoonekana kama hatua kali kuwahi kuchukuliwa na Uturuki kuhusiana na machafuko hayo, Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, rafiki wa Rais Assad, ameishutumu Syria, kutokana na ghasia hizo ambazo zimesababisha zaidi ya watu 3,000 kukimbilia katika eneo la mpaka.

Mmwandishi: Grace Patricia Kabogo (AFPE,RTRE)
Mhariri: Mohamed Dahman