1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri kuadhimisha miaka 75 tangu kuundwa kwa NATO

4 Aprili 2024

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, wanakutana leo kuadhimisha miaka 75 tangu kuundwa kwa muungano huo wa kijeshi.

https://p.dw.com/p/4ePGT
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO katika siku ya kwanza ya mkutano wao mjini Brussels. Picha: Geert Vanden Wijngaert/AP Photo/picture alliance

Katika siku ya pili ya mkutano wao unaofanyika mjini Brussels, mawaziri hao watakusanyika kwa halfa ya kukumbuka kutiwa saini kwa mkataba ulioanzisha mfungamano huo wa kijeshi  mnamo Aprili 4 mwaka 1949.

Jumuiya ya NATO iliasisiwa na nchi 12 kwa dhima ya kutoa uhakika wa usalama mbele ya kitisho cha uliokuwa Muungano wa Kisovieti.

Miaka 75 baadaye idadi hiyo imefikia wanachama 32 chombo hicho na kimechukua tena jukumu muhimu kwenye masuala ya ulimwengu hasa tangu Urusi ilipoivamia kijeshi Ukraine.

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, amesema umuhimu wa mshikamano baina ya nchi wanachama unaongezeka katika wakati ulimwengu unashuhudia wimbi la machafuko na mivutano.