1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Mawaziri wa fedha wa G7 kujadili vikwazo zaidi kwa Urusi

23 Februari 2023

Mawaziri wa fedha kutoka kundi la mataifa saba yalioendelea kiuchumi duniani, G7, wanatarajiwa kujadili uwezekano wa kuiwekea Urusi vikwazo vipya, na kuongeza msaada kwa Ukraine

https://p.dw.com/p/4Ns9V
Deutschland | Pressekonferenz | Treffen der G7-Minister für Klima, Energie und Umwelt
Picha: Annegret Hilse/REUTERS

Mawaziri wa fedha kutoka kundi la mataifa saba yalioendelea kiuchumi duniani, G7, wanatarajiwa kujadili uwezekano wa kuiwekea Urusi vikwazo vipya, na kuongeza msaada kwa Ukraine, siku moja kabla ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi.

Soma pia:Kansela wa Ujerumani Scholz kuhudhuria mkutano wa G7 Ijumaa

Waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire, amesema kabla ya mazungumzo yao mjini Bengaluru, India, kwamba hatua zilizochukuliwa mpaka sasa zimefanikiwa kupunguza kwa nusu mapato ya mafuta ya Urusi, na kuzivuruga kabisaa sekta za kimkakati kama usafiri wa anga na magari.

Alisema mkutano wa leo unaomjumuisha pia waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen, unapaswa kujadili mpango mpya wa dola bilioni 16 wa shirika la fedha duniani, IMF, kwa ajili ya Ukraine kwa kipindi cha miaka minne. Afisa mwandamizi wa serikali ya Marekani alisema wiki iliyopita kwamba Marekani na washirika wake wa G7 walipanga kutangaza awamu mpya kubwa ya vikwazo karibu na kumbukumbu ya Februari 24, zikiwemo hatua dhidi ya wakewapaji wa vikwazo vya sasa.