Mawaziri wa G20 waikosoa uvamizi wa Urusi, Ukraine
22 Februari 2024Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron amesema kwenye kikao cha ndani kwamba Urusi inatakiwa kuwajibika kwa uvamizi huo, hayo ikiwa ni kulingana taarifa iliyotolewa na ofisi yake.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Australia, Canada, Ujerumani, Italia, Ufaransa na Norway pia walitoa maoni kama hayo katika siku ya kwanza ya mkutano huo wa siku mbili.
Soma pia:Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G20 wakutana Brazil
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide(ESPEN BART AIDA) aliwaambia waandishi wa habari kwamba mwenzao wa Urusi Sergei Lavrov alimjibu Cameron kwa utulivu kwa orodha ya hoja kinzani kuhusiana na kile kinachoendelea nchini Ukraine.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock kwa upande wake alitoa wito kwa kundi hilo kushinikiza kuhusu suluhu katika vita hivyo na kwenye mzozo wa Mashariki ya Kati.