Mawaziri wa mambo ya nje wa EU wakutana Brussels
16 Desemba 2024Matangazo
Kikao hicho ambacho kitaongozwa kwa mara ya kwanza na mkuu mpya wa sera za nje wa Umoja huo wa Ulaya, Katja Kallas, pia kinajiandaa kuidhinisha duru ya 15 ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi tangu nchi hiyo ilipovamia Ukraine Februari 2022.
Waziri wa mambo ya nje wa ukraine Andrii Sybiha nae pia anatarajiwa kushiriki mkutano huo kwa njia ya video kutowa sura ya hali ilivyo kwa sasa katika uwanja wa vita.
Kadhalika mkutano huo unafanyika wakati suala la uwezekano wa Umoja wa Ulaya kuhusika katika kupeleka kikosi cha kulinda amani, likipata nguvu.