1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yaingia mkwamo

10 Julai 2024

Mazungumzo ya kutafuta amani ya Sudani Kusini ambayo yalikuwa karibu kufikia mwisho yanakabiliwa na mkwamo baada ya makundi ya upinzani kutoa matakwa mapya.

https://p.dw.com/p/4i6WW
Sudan Kusini | Rais Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Picha: Samir Bol/ZUMAPRESS/picture alliance

Miongoni mwa matakwa hayo wakishinikiza kufutwa kwa muswada mpya wa sheria unaoruhusu watu kukamatwa bila waranti wa mahakama. 

Wawakilishi wa upinzani kwenye mazungumzo hayo yanayofanyika nchini Kenya tangu mwezi Mei wamesema muswada huo ni lazima kwanza ufutwe kabla ya wao kutia saini makubaliano ya amani. 

Mwakilishi wa upinzani Pagan Amum Okiech amewaambia waandishi habari jana Jumanne kwamba litakuwa jambo lisilo na maana kuuridhia mkataba wa amani ikiwa Rais Salva Kiir atautia saini muswada huo kuwa sheria.

Soma pia:Changamoto mpya kwa wakimbizi wa Sudan nchini Chad
Mapema wiki iliyopita Bunge la Sudani Kusini lilipitisha muswada huo wa sheria na rais Kiir anao muda wa siku 30 kuutia saini ili uwe sheria kamili. Wakosoaji wake wanasema sheria hiyo itakiuka haki za msingi za binadamu na uhuru wa umma Sudan Kusini. 

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetolea mwito rais Kiit kutoutia saini muswada huo likisema linahujuma haki za watu na kuimarisha taasisi za dola ambazo zina historia ya kufanya ukandamizaji