Mazungumzo ya mkataba wa kushughulikia majanga yaanza tena
5 Novemba 2024Wakati wa ufunguzi wa mazungumzo hayo, katibu mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, aliwaambia waakilishi wa mataifa hayo kwamba wanakabiliwa na jukumu la kukamilisha majukumu yao kwa wakati ufaao na pia kufikia makubaliano madhubuti.
Ghebreyesus aonya janga litakalofuata halitasubiri mazungumzo
Ghebreyesus, aliongeza kuwa muda umeyoyoma na kwamba virusi vya Uviko19 bado vinasambaa, ugonjwa wa mpoxni dharura ya kimataifa ya afya na kwamba pia kuna mripuko wa ugonjwa wa marburg na H5N1, akiongeza kuwa janga litakalofuata halitasubiri.
Ugavi wa chanjo kujadiliwa baadaye
Baada ya zaidi ya miaka miwili ya mazungumzo, matumaini ni makubwa ya kukamilisha makubaliano hayo ifikapo Novemba 15, ingawa suala kuu la jinsi ya kugawanyachanjo linatarajiwa kufanyiwa kazi baadaye.