Mazungumzo ya Urusi na Ukraine kuanza Istanbul
28 Machi 2022Hata hiyo taarifa hiyo hakuwa na ufafanuzi zaidi, ingawa katika mazungumzo yao kwa njia ya simu ya jana Jumapili, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na mwenziwe wa Urusi Vladimir Putin walikubaliana kufanyika kwa mazungumzo hayo ya Istanbul ambayo serikali ya Ankara ina matumani kuwa yanaweza kufanikisha hatua ya kuwekwa chini kwa mtutu wa bunduki.
Lakini awali kabla ya taarifa hiyo mmoja wa maafisa waandamizi wa Ukraine, mshauri katika wizara ya mambo ya ndani, akiwa pia mwakilishi wa Ukraine katika mazungumzo hayo Vadym Denysenko ametoa kauli ya kukatisha tamaa akisema hataraji matokeo makubwa ya kupatikana katika mazungumzo hayo.
Kugundulika kwa mabomu katika eneo la Bahari Nyeusi
Katika eneo la mapigano Uturuki imesema imegundua mabomu yalitogwa katika eneo la Bahari Nyeusi, katika ukanda wa pwani ya Igneada, karibu kabisa na mpaka wa Bulgaria. Taarifa hiyo ya wizara ya ulinzi iliyosambazwa kupitia ukurasa wake wa Twitter inatolewa baada ya kugundulika safari nyingine kama hiyo ya kile kinachodhaniwa safari za meli zilizodumu kwa takribani masaa manee katika eneo la Ujia wa Bahari wa Bosporous.
Kimsingi Uturuki vilevile imezuia shughuli za uvuvi katika nyakati za usiku katika eneo lake la bahari la kaskazini/magharibi hadi itakapoamua vinginevyo. Lakini hata hivyo haijaweza kufahamika mara moja kama mabomu hayo yana uhusiano wa vita vinavyoendelea nchini Ukraine. Lakini Urusi na Ukraine zimekuwa zikitupiana lawama za kutega mabomu katika eneo la Bahari Nyeusi.
Watu 160,000 wanaelezwa kukamwa katika mji uliozingirwa wa Mariupol
Watu 160,000 bado wamekwama katika mji uliozingirwa wa Mariupol, huku kukiwa bado kuna shida kadhaa ikiwemo ya umeme. Naibu waziri mkuu anasema kwa mujibu wa taarifa kutokaUrusihakuna milango iliyo wazi kwa ajili ya misaada ya kiutu katika mji huo wa bandari. Mkuu wa idara ya kijasusi ya Ukraine anasema Urusi inajaribu kuligawanya taifa la Ukraine katika mapande mawili, baada ya kushindwa kulidhibiti taifa zima. Akimaanisha kuwe na eneo linalodhibitiwa na Urusi na lile katika udhibiti wa serikali ya Ukraine.
Ofisi yenye kushughulika na haki za binaadamu katika Umoja wa Mataifa inaasema watu 1,119 wameuwawa na wengine 1,790 wamejeruhiwa tangu kuzuka kwa mapigano nchini Ukraine.
Vzanzo: RTR/DPA