1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamala Harris aingia kwenye kampeni za Urais

23 Julai 2024

Baada ya kupata uungwaji mkono kutoka kwa vigogo wa chama cha Democratic, Kamala Harris atajaribu uwezekano wake wa kushawishi wapiga kura kwenye mkutano wa kampeni huko Wisconsin

https://p.dw.com/p/4icvV
Kamala Harris
Mgombea wa chama cha Democratic Kamala Harris Picha: Hu Yousong/picture alliance

Wisconsin ni jimbo lenye nguvu za kushawishi matokeo ya uchaguzi kwa uwezekano wake wa kukabiliana na Donald Trump.

Katika mkutano wa kampeni wa  usiku wa Jumatatu usiku huko Delaware, mgombea huyo wa miaka 59 alionjesha umma namna ya muonekano wake ugombea.

" Kwa hivyo katika siku na majuma yajayo, binafsi  pamoja nanyi, nitafanya kila niwezalo kuunganisha chama chetu cha Kidemokrasia, kuunganisha taifa letu. Ili katika siku 106 tuwe na jukumu la kutimiza, tuna nyumba za kubisha hodi, tuna watu wa kuzungumza nao, tuna simu za kupiga, na tuna uchaguzi wa kushinda.

Kamala Harris aanzisha kampeni ya Urais 2024

Makamu wa rais, ambaye amechukua nafasi ya Joe Biden katika mojawapo ya tafrani kubwa zaidi ya uchaguzi katika historia ya kisasa ya Marekani, ana chini ya miezi minne tu, katika kuwashawishi umma wa Marekani kwamba ana kile kinachohitajika kwa ofisi ya juu zaidi ya taifa hilo.