1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo mkubwa wafanyakazi wa reli umeanza Uingereza

21 Juni 2022

Mgomo mkubwa wa usafiri wa reli kwa takribani miaka 30 umeanza leo nchini Uingereza ambapo maelfu ya wafanyakazi wameingia mitaani kupinga malipo duni na kupunguzwa kazi.

https://p.dw.com/p/4D07D
Symbolbild I Streik in England
Picha: Vuk Valcic/ZUMA/dpa/picture alliance

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, ambaye yupo katika shinikizo la kuwasaidia raia wake, wanaokabiliwa na hali ngumu zaidi ya kiuchumi katika miongo kadhaa amesema hatua ya migomo ya kiviwanda itaathiri hali ya kibiashara nchini humo katika kipindi hiki ambacho taifa linajitahidi kujiondoa katika athari za janga la virusi vya corona.

Vyama vya wafanyakazi vimesema mgomo huo utaonesha mwanzo wa hali ya kutoridhika kutokana na hali jumla ilivyo kwa sekta nyingine kama ualimu, watoa tiba, wahudumu katika usafi na kwengineko kutokana na kile kinachoelezwa kuwa kupanda kwa bei ya vyakula na mafuta, hali inayofanya mfumuko wa bei kufikia asilimia 10.

Hali ngumu ya maisha kwa wafanyakazi wa sekta ya afya.

Katibu Mkuu wa chama cha Wafanyakazi wa Reli, Majini na Uchukuzi (RMT), Mick Lynch amesema mfanyakazi wa Uingereza anahitaji nyongeza ya mshahara. Wanahitaji uhakika wa ajira, mazingira mazuri na mkataba wenye usawa kwa ujumla wake. Amesema kama watavipata hivyo hawatauvuruga uchumi wa Uingereza kwa wakati huu, hali ambayo inaweza kuendelea katika kipindi chote cha msimu wa kiangazi.

Symbolbild I Streik in England
Abiria waliokwama kutokana na mgomo wa treni LondonPicha: Jenny Goodall/Daily Mail/picture alliance

lakini Waziri Mkuu wa Jonhson ambae anayapinga maandamano hayo anasema kuendelea kwake kutaathiri kazi za wafanyakazi wa shirika la reli, kuathiri biashara na jamii katika maeneo yote ya nchi. Kwa mujibu wa ofisi yake anasema atatoa taarifa kwa baraza lake la mawaziri leo hii.

Serikali ya Uingereza imekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa wabunge wa upinzani kwa kukataa kuhusika katika mazungumzo ya kusuluhisha mzozo huo. Mawaziri wanasema ni suala la vyama vya wafanyakazi kulifanyia kazi moja kwa moja na waajiri wa reli.

Soma zaidi: Wakuu wa Afrika Mashariki wakubali kupeleka jeshi, DRC

Mapema mwezi huu utafiti wa wachambuzi wa asasi iitwayo  YouGov iliyowekwa hadharabni ulisema maoni ya watu kuhusu mgomo huo yamegawanyika, takribani nusu ya waliohojiwa wanapinga kitendo hicho huku zaidi ya theluthi wakiunga mkono. Leo Rudolph, wakili mwenye umri wa miaka 36 ambaye alitembea kwenda kazini, amesema atakuwa na kinyongo zaidi kadiri mzozo unavyoendelea.

Mgomo huu wa reli unamaanisha ni nusu tu ya mtandao wa usafri wa treni nchini Uingereza utaendelea kufanya kazi kama kawaida katika siku za mgomo kwa kupunguza hudumua katika njia zake.

Chanzo: RTR