1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mhubiri Mmarekani akamatwa Rwanda kwa 'kuvuruga utulivu'

8 Oktoba 2019

Mhubiri wa Kimarekani ambaye alitarajiwa kufanya kikao na waandishi wa habari mjini Kigali, amekamatwa na polisi mjini humo kwa madai ya kuvuruga utulivu.

https://p.dw.com/p/3QsWu
Ruanda Kigali Straße Soldat Wahl 2010
Picha: picture alliance/dpa

Polisi ya Rwanda imemkamata mhubiri wa Kimarekani ambaye alitarajiwa kufanya kikao na waandishi wa habari mjini Kigali jana na ambaye kituo chake cha redio nchini humo kilifungwa na mamlaka mwaka jana.

Msemaji wa polisi John Bosco Kabera aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa Gregg Schoof alikamatwa kwa kuvuruga utulivu.

Maafisa nchini Rwanda mwaka jana walikifunga kituo cha redio kilichomilikiwa na Schoof, cha Amazing Grace baada ya kurusha hewani mahubiri ambayo wanaharakati wa haki za wanawake walisema yalieneza chuki dhidi ya wanawake. Mahubiri hayo yaliwaelezea wanawake kuwa watu wabaya sana.

Schoof alitaka kuwahutubia wanahabari kabla ya kuondoka nchini humo lakini akakamatwa na polisi katika sehemu ambayo kikao hicho cha wanahabari kilitarajiwa kufanyika. Alikabidhiwa kwa Idara ya Upelelezi ya Rwanda ili kuhojiwa zaidi.