Milan. Itali yataka kukamatwa maajenti wengine wa CIA.
20 Julai 2005Mwendesha mashtaka nchini Itali ameitaka mahakama leo kutoa hatia ya kuwakamata wafanyakazi sita zaidi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA wanaotuhumiwa kuhusika katika kumteka nyara kiongozi mmoja wa dini ya Kiislamu , mwenye imani kali katika mitaa ya mji wa Milan hapo 2003.
Itali tayari imetoa hati za kukamatwa wakala 13 miongoni mwa wakala 19 wa shirika hilo la ujasusi ambao wanasema walihusika katika operesheni ya siri ya kumteka nyara kiongozi huyo raia wa Misr Abu Omar, na kumkabidhi kwa maafisa wa serikali ya Misr kwa ajili ya mahojiano.
Msaidizi huyo wa mwendesha mashtaka Armando Spataro ameitaka mahakama ya rufaa mjini Milan kuwakamata wakala wengine sita waliobaki kuhusiana na kuhusika kwao katika kupanga utekaji nyara huo, tukio lililochafua uhusiano kati ya Itali na Marekani.