1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Mimi pia ni binaadamu, nina hisia"

26 Mei 2014

Mbiu ya Mnyonge inasimulia hadithi ya mtoto Hassani na wenzake wenye ulemavu wa ngozi kwenye kituo cha Skuli Maalum ya Msingi ya Buhangija, Tanzania, wakisema nao pia ni wanaadamu, wana hisia, wana ndoto na wana roho.

https://p.dw.com/p/1C6m4
08.01.2015 DW Global 3000 Albino Mädchen

Kwa mwaka wa tano sasa, mvulana Hassani Hamisi mwenye umri wa 16 amehifadhiwa kwenye Skuli Maalum ya Msingi ya Buhangija, lakini - kama walivyo wenzake kadhaa miongoni mwa watoto 176 wenye ulemavu wa ngozi kituoni hapo - hajawahi kutembelewa na mzazi wake.

Mohammed Khelef anaangazia jaala ya watoto hao ambayo ni kielelezo cha mchanganyiko wa hofu na matumaini.

Kusikiliza makala haya, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Mohammed Khelef
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman