Miripuko yailenga ghala la maroketi nchini Syria
13 Agosti 2023Limelinukuu shirika la haki za binadamu linalofuatilia habari za vita likisema kuwa milipuko hiyo ililenga na kuharibu ghala la kuhifadhi roketi llinalomilikiwa na makundi yanayoiunga mkono serikali ya Iran.
Soma pia: Watu wenye silaha waua askari 23 Syria
Tukio hilo linafuatia shambulio jingine la anga la Jumatatu iliyopita lililofanywa na Israel karibu na Damascus. Wanajeshi wanne wa Syria na wapiganaji wawili wanaoiunga mkono serikali ya Iran waliuwawa kwenye shambulio hilo.
Iran imekuwa mshirika mkubwa wa Rais Bashar al Assad katika miaka 12 ya mzozo wa Syria. Wapiganaji ambao ni mawakala wa Iran kwenye vita hivyo, kundi la Hezbollah la Lebanon ma makundi ya Iraq yanayoiunga mkonono Tehran yanashikilia sehemu kubwa za mashariki, kusini na kaskazini mwa Syria pamoja na vitongoji vinavyouzunguka mji mkuu.