Misri na India zasaini mikataba ya kuimarisha mahusiano
26 Juni 2023Viongozi hao wawili walisaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zao na kuwa kile kilichoitwa ushirikiano wa kimkakati, ikimaanisha nchi hizo zimeridhia kuongeza ushirikiano na kuwa na mikutano ya mara kwa mara, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa.
Soma pia: India yaiombea Afrika uanachama wa kudumu, G20
Modi ni waziri mkuu wa kwanza wa India kufanya ziara ya kiserikali nchini Misri katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili. Aliwasili Jumamosi mjini Cairo na ziara hiyo ya siku mbili imekuja miezi sita baada ya rais El Sisi kuitembelea India akiwa kama mgeni rasmi wa heshima katika siku ya kumbukumbu ya Uhuru wa India.
Serikali hizo mbili pia zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta za kilimo, utafiti wa masuala ya akiolojia, vitu vya kale na sheria.