1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Misri yafanya mkutano wa kilele wa nchi za Kiislamu - D8

19 Desemba 2024

Misri imekuwa mwenyeji wa viongozi wa Uturuki na Iran kwa mkutano wa kilele wa nchi nane zenye Waislamu wengi kujadili msukosuko wa kikanda ukiwemo mzozo wa Gaza na machafuko nchini Syria.

https://p.dw.com/p/4oNBw
Mkutano wa D-8 Cairo, Misri
Mkutano huo wa D-8 unayajumuisha pia mataifa mengine kama Nigeria, Pakistan, Bangladesh, Indonesia na Malaysia.Picha: Iranian Presidency/Zuma/IMAGO

Misri imekuwa mwenyeji wa viongozi wa Uturuki na Iran kwa mkutano wa kilele wa nchi nane zenye Waislamu wengi, dhidi ya hali ya msukosuko wa kikanda ukiwemo mzozo wa Gaza na machafuko nchini Syria.

Mkutano huo wa Shirika la D-8 la Ushirikiano wa Kiuchumi, linalojulikana ´pia kama "Developing-8," unayajumuisha pia mataifa mengine kama Nigeria, Pakistan, Bangladesh, Indonesia na Malaysia.

Katika mkusanyiko huko kutakuwa na kikao maalum kuhusu Gaza na Lebanon, ambacho kitahudhuriwa na rais wa Palestina Mahmoud Abbas. Mkutano huo utawakutanisha marais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Masoud Pezeshkian wa Iran kwa mara ya kwanza tangu rais wa Syria Bashar al-Assad aondolewe madarakani.