Mjadala wa Kidini - Daraja la Mto Gori
1 Juni 2011Hayo yanadhihirika katika tamthilia yetu ya ‘Katika Daraja la Mto Gori'.
Imani ni nguzo muhimu katika maisha ya kila siku ya wanawake na wanaume wengi wa Kiafrika,vijana kwa wazee,masikini na matajiri.Wakazi wa bara la Afrika ni waumini wa dini tatu kuu ulimwenguni zilizo na misingi ya kumuamini Mungu mmoja yaani-Uislamu,Ukristo na Uyahudi-zinawafuasi wake pamoja na imani za dini za kitamaduni,jambo linaloashiria utajiri wa jamii hizo.
Hatahivyo,katika mji mdogo wa Gori,imani na dini tofauti za wakazi wake huenda zikawa chachu ya kusababisha purukushani.Mto unaoguwanya mji huo ulio na soko maarufu unazigawa pia jamii mbili mashuhuri:ya Dembele na Omer.Jamii ya Dembele ni ya Wakristo na Omer ni Waislamu.Uhasama wa jadi baina ya jamii hizo mbili unasadikika kuwa umepangiwa hivyo.
Hilo huenda likabadilika baada ya Harry Dembele kukutana na Layla Omer.Vijana hao ni wanafunzi wa Chuo cha Ubuntu,kinachounga mkono imani na dini tofauti pamoja na madhehebu mbalimbali,kinachowaleta pamoja vijana wa umriwa miaka 16 hadi 18 wa kike na kiume.
Kwa kuzikiuka dhana zote na fikra nzito za tofauti zao,vijana hao wawili Layla na Harry wanajifunza umuhimu wa majadiliano,ushirikiano na kuvumiliana.
Jee,penzi lao lililopigwa marufuku lina uwezo wa kunawiri ukiyazingatia yote hayo?
Michezo ya Noa Bongo:Jenga Maisha yako inaweza kusikilizwa katika lugha sita tofauti: Kiswahili, Kiingereza,Kifaransa,Kihausa,Kireno na Kihabeshi.Mradi huu unaungwa mkono na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani.