Mwandishi wa DW Edith Kimani ameitembelea nchi ya Ghana na safari yake inaanzia katika Black Star Square ambapo anakutana na Bernice Asiedu mwalimu wa mazoezi. Tazama vidio hii inayoonesha jinsi msichana huyu anavyojaribu kuufanya mji wa Accra uwe Mji Mkuu wa mazoezi Afrika na pia mji ambao watu wanakula vyakula vinavyochangia katika kuleta afya bora.