1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Mkataba wa kusafirisha gesi ya Urusi kwenda EU umekamilika

1 Januari 2025

Usambazaji wa gesi ya Urusi kwenda mataifa ya Ulaya kupitia Ukraine umesitishwa leo baada ya mkataba wa miaka mitano kati ya kampuni ya usafirishaji wa gesi ya Ukraine Naftogaz na ile ya Urusi Gazprom kukamilika.

https://p.dw.com/p/4ojDc
Gazprom | Gesi ya Urusi
Bomba la kusafirisha gesi ya UrusiPicha: ITAR-TASS/IMAGO

Hatua hiyo inamaliza muongo mmoja wa uhusiano mbaya kati ya Urusi na Ukraine uliochochewa na Urusi kuchukua eneo la rasi ya Crimea kutoka kwa Ukraine mwaka 2014. Ukraine baadaye ilisimamisha ununuzi wa gesi kutoka Urusi mwaka uliofuata.

Waziri wa nishati wa Ukraine German Galushchenko amesema tayari wameyafunga mabomba yanayosafirisha gesi ya Urusi kupitia ardhi yake na kueleza kuwa uamuzi huo ni tukio la kihistoria.

Soma pia: Urusi yasema nchi za Ulaya zitalipa zaidi kwa ajili ya mahitaji ya gesi 

Galushchenko amesema hatua hiyo itaisabibishia Moscow hasara kubwa.

Kufungwa kwa mabomba hayo ya kusafirisha gesi kulitarajiwa kutokana na uvamizi wa Urusi mnamo Februari 2022 huku Ukraine ikiweza wazi kwamba haitaongeza mkataba huo.