1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkenya Peter Tabishi ashinda tuzo ya mwalimu bora duniani

Josephat Charo
24 Machi 2019

Mwalimu wa hesabu na fizikia kutoka shule moja ya sekondari katika kijiji kinachopatikana eneo la bonde la ufa nchini Kenya, ameshinda tuzo ya mwalimu bora mwaka 2019 ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/3Fb0S
Vereinigte Arabische Emirate, Dubai - Ein kenianischer Lehrer für Naturwissenschaften gewann einen Preis im Wert von 1 Million Dollar
Mwalimu kutoka Kenya, Peter Tabichi, katikati, muigaji filamu Hugh Jackman, kushoto na mrithi wa mfalme wa Dubai, mwanamfalme Sheikh Hamdan bin Mohammed Al Maktoum, kulia, baada ya Tabichi kushinda dola milioni moja za tuzo ya mwalimu bora Dubai, Falme za Kiarabu, Jumapili Machi 24, 2019.Picha: picture-alliance/J. Gambrell

Peter Tabishi, ambaye waandaaji wanasema hutoa asilimia 80 ya mshahara wake wa mwezi kwa watu masikini, amepokea tuzo hiyo katika sherehe iliyofanyika siku ya Jumamosi huko Dubai, ambayo mwenyeji wake alikuwa nyota wa filamu kutoka Hollywood, Hugh Jackman.

"Kila siku barani Africa tunafungua ukurasa mpya wa maisha. Tuzo hii hainitambui mimi bali inawatambua vijana wa bara hili. Nipo hapa kwa sababu ya kile ambacho wanafunzi wangu wamefanikiwa katika maisha yao," alisema Tabishi.

"Tuzo hii inawapa wao fursa. Inauambia ulimwengu kwamba wanaweza kufanya kitu chochote," aliongeza kusema mwalimu huyo baada ya kuwashinda walimu wengine tisa kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu waliofanikiwa kufika fainali kuwania tuzo hiyo ya mwalimu bora.

afpe