1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkopo IMF

Sudi Mnette/AFPE25 Machi 2009

Kutokana na kundelea kwa kasi za athari za Mgogoro wa Kiuchumi Shirika la fedha Duniani limezindua mpango maalum wenye masharti nafuu kwa lengo la kuzisidia nchi zinazokua vyema kiuchumi

https://p.dw.com/p/HJLy
Mkurugenzi wa IMF Dominique Strauss-KahnPicha: AP

Hatua hiyo imekuja wiki moja kabla ya mkutano mkubwa wa nchi zilizoendelea kiviwanda Duniani unaotarajiwa kufanyika mjini London,nchini Uingereza.

Mpango huo wakichumi unaojulikana kwa ufupi kamaFCL utachukua nafasi ya uliyokuwepo wa muda unaokaribiana na huo wa SLF ambao tangu kuundwa kwake oktoba mwaka jana haujaweza kuonesha mafanikio.

Katika utaratibu huu wa sasa nchi husika inaweza kupata kiasi cha fedha kwa kipindi kisichopungua cha miezi sita au 12 baada ya kumaliza taratibu za maombi.

Katika mpango huo Shirika la fedha Duniani IMF limetenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuzikopesha nchi wanachama zipatazo 185 Duniani kote utaratibu ambao umetajwa kuweza kuzikwamua kiuchumi nchi husika.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo mjini Washington Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Dominique Straus-Kahn alisema kwamba mkopo huo unatokana na mabadiliko muhimu ya kiuchumi kwa nchi Wanachama na hasa katika kipindi hiki cha mgogoro wa kiuchumi.

Amesema mabadiliko ya utaratibu uliyopo utamuwezesha mkopaji kupata matokeo ya maombi yake haraka kuliko ilivyokuwa awali na vipaumbele vitatolewa kwa nchi ambazo zinaathirika zaidi.

Strauss-Kahn amezitaka nchi ambazo zimeathirika kwa kiasi kikubwa kutumia mpango huo ili kuweza kuwanusuru wananchi wake na makali ya hali mbaya.

Mchumi mmoja kutoa Brazil Arberto Ramos amesema mkopo huo umeonesha maendeleo makubwa katika mipango ya utoaji mikopo mikubwa ya muda mfupi.

Amesema vigezo vilivyoahinishwa, nchi za Amerika ya Kusini kama Brazil,Chile,Colombia na Peru bila shaka zitaweza kutimiza masharti ya kupata mkopo huo wakati nyingine kama Argentina,Ecuador hazitaweza kufikia vigezo.

Kwa mujibu wa IMF wa katika mkutano wa G20 wa aprili 2 miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa kwa kiasi kikubwa ni pamoja na mpango huo wa kuinua uchumi ambao pia wahusika wakuu kutoka shirika hilo na Benk ya Dunia wanatarajiwa kushiriki.

Katika kuchangia mfuko huo wa Fedha Duniani Japan mwezi uliyopita imechangia bilioni 100,Umoja wa Ulaya wiki iliyopita uliahidi kutoa bilioni 75 na Marekani akiwa kama mbia mkuu wa mfuko huo ametaka fedha za dharula kuongozwa kufikia dola bilioni mia tano pasipo kutaja kiwango ambacho itachangia

Mamilioni ya watu wameathirika tangu kuanza kwa Mgogoro wa Kichumi Duniani ambapo baadhi yao wamepteza ajira na wengine hata kukosa makazi na hasa nchini Marekani.

Historia inaonesha mabadiliko hayo makubwa kufanywa na IMF yanatokana na kuporomoka kwa uchumi kwa kiasi kikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya duniani.