Mkutano kati ya AU na UU-Lisbon
9 Desemba 2007LISBON:
Katika mkutano wa kilele wa siku 2 kati ya Umoja wa Ulaya na Afrila mjini Lisbon,Ureno,Kanzela Angela Merkelwa Ujerumani, amesema kwamba rais Robert Mugabe wa Zimbabwe anaichafua heba ya bara la Afrika.Akaongeza kusema kwamba, Zimbabwe inamtia wasi wasi kila mmoja barani ulaya na Afrika.Akawataka viongozi wa Afrika kupigania demokrasia isonge mbele nchini zimbabwe.
Kanzela Merkel akaongeza:
„Wakati unapita na hali za wananchi zazidi kuwa mbaya.
Labda huu ni mchango mdogo tu ikiwa mabadiliko huko yatatokea haraka.“
Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, anaususia mkutano wa Lisbon kutokana na kuhudhuria kwa rais Mugabe.
Viongozi wengine wa Ulaya, hawakujiunga na Uingereza kususia mkutano wakidai kwamba, mazungumzo nae ndie njia bora kabisa ya kukabiliana na matatizo ya zimbabwe kama vile rekodi ya rais Mugabe ya kukanyaga haki za binadamu.
Viongozi wa Ulaya na Afrika kutoka jumla ya nchi 67, wanafanya mkutano wao wa kwanza wa kilele tangu kupita miaka 7.Lengo lake, ni kuunda mkakati mpya wa ushirikiano baina ya mabara haya 2.Mkutano unatazamiwa kumalizika leo kwa tangazo la pamoja juu ya mkakati huo.Kuhusu ushirikiano huu rais wa Ghana John Koufour alisema:
„Afrika inaihitaji Ulaya sawa na Ulaya inavyoihitaji Afrika.“
.