Mkutano kuhusu uchumi waendelea mjini Davos
25 Januari 2008Matangazo
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema nchi tajiri zinashindwa kutimiza majukumu yao kwa watu maskini na zinapaswa ziongeze juhudi kukabiliana na athari za umaskini duniani. Ban Ki Moon alikuwa akizungumza katika mkutano kuhusu uchumi unaoendelea mjini Davos nchini Uswisi.
Yeye pamoja na muimbaji mashuhuri wa muziki wa miondoko ya Rock, Bono, na muasisi wa kampuni ya kompyuta ya Microsoft, Bill Gates, wamefaulu kuubadili mkondo wa mkutano wa Davos ambao kitamaduni hujadili mada kama vile uchumi wa dunia. Mkutano huo unajadili maswala mbalimbali yakiwemo ugonjwa wa malaria.