1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano mkuu wa wananchi wa China

5 Machi 2013

Waziri mkuu anaemaliza wadhifa wake aahidi ukuaji wa kiuchumi wa 7.5 asili mia mwaka huu

https://p.dw.com/p/17qWy
Waziri mkuu Wen Jiabao (kushoto) akipeana mkono na makamo wake na mrithi wake Li KeqiangPicha: Reuters

China inalenga ukuaji wa kiuchumi wa asili mia 7.5 kwa mwaka huu.Lengo hilo limetangazwa na waziri mkuu anaemaliza wadhifa wake Wen Jiabao,alipokuwa anafungua mkutano mkuu wa wananchi wa China hii leo.Wakati huo huo serikali imetangaza nyongeza kubwa ya gharama za kijeshi.Akijitokeza kwa mara ya mwisho kama kiongozi wa serikali,Wen Jiabao ametetea sera za serikali yake zinazozidi kukosolewa nchini humo.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 70 atamkabidhi  kijana,hatamu za uongozi wa nchi hiyo.

Kwa mara ya mwisho Wen amesimama mbele ya jukwaa ambalo halijapambwa kwa mauwa,na kuwahutubia wawakilishi karibu 3000 katika ukumbi mkubwa wa umma-sababu ya hayo ni kwamba chama kimeamua kuachana na makuu.Hata hivyo Wen amejitahidi awezevyo kusifu ufanisi wa shughuli za serikali yake:

Serikali ishughulikie zaidi usafi wa mazingira

Volkskongress China 2013
Mjumbe anasinzia wakati wengine wanashangiria mkutanoniPicha: Reuters

Wen Jiabao anasema:Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,uongozi,kutokana na changamoto kubwa na hali tete ya kiuchumi ulimwenguni,ulilazimika kupitisha maamuzi yaliyoiwezesha China kuepukana na vishindo kutoka nje.Maarifa yameonyesha maamuzi yalikuwa sahihi kabisa."

Wakati huo huo Wen ameitumia fursa hiyo kuwakosoa wale wanaohoji kwamba ukuaji wa kiuchumi wa China si sawia na si wa kudumu.Kwa mwaka huu tulio nao Wen anakadiria ukuaji wa kiuchumi wa asili mia 7.5Lakini anasema juhudi zaidi zinahitajika ili kulifikia lengpo hilo.Wen Jiabao ameitaka serikali mpya iwajibike zaidi katika ulinzi wa mazingira.

Mada nyengine muhimu inayoikabili serikali mpya inahusiana na juhudi za kupambana na rushwa.Wen hakuzungumzia umuhimu wa mageuzi ya kisiasa.Hata hivyo ametangaza kuongezeka kwa gharama za kijeshi mwaka huu hadi kufikia Eureo bilioni 88.

Mwishoni mwa mkutano huo mkuu utakaodumu wiki mbili,Wen Jiabao atamkabidhi hatamu za uongozi aliyekuwa hadi wakati huu makamo waziri mkuu Li Keqiang.Kwa upande wake rais Hu Jiantao atamkabidhi wadhifa huo,kiongozi mpya wa chama na jeshi Xi Jinping.

Mwandishi:Kirchner,Ruth/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Mohammed  Abdul-Rahman