Mkutano mpya wa amani DRC kufanyika Luanda
2 Desemba 2024Matangazo
Mkutano huo utahudhuriwa na marais wa Rwanda Paul Kagame na Félix Tshisekedi wa Kongo.
Hayo yametangazwa hivi leo na ofisi ya rais wa Angola na kusema mkutano huo uliitishwa na rais Rais wa Angola Joao Lourenço ambaye aliteuliwa na Umoja wa Afrika kuwa mpatanishi, na ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kutafuta suluhu ya kudumu kwenye mzozo huo.
Mapema mwezi Agosti, Rwanda na DRC zilitia saini makubaliano tete ya kusitisha mapigano na ziliidhinisha hivi karibuni nyaraka muhimu kwa ajili ya kuendeleza mchakato huo wa amani mashariki mwa Kongo, eneo linalokumbwa na uasi wa makundi kadhaa yenye silaha.