MKUTANO WA KILELE KATI YA PUTIN,CHIRAC NA SCHRÖDER HUKO SOTSCHI,URUSI NDIO MADA KUU YA UCHAMBUZI WA WAHARIRI WA MAGAZETI YA LEO YA UJERUMANI:
1 Septemba 2004GAZETINI: 01-09-04
Gazeti la jiji la Cologne-KÖLNISCHE RUNDSCHAU laandika kuhusu mkutano wa kilele wa Tsochi kati ya rais Putin,Chirac na kanzela Schröder:
"Kwa mkutano wao 4 huko Tsochi, vigogo hivyo 3 vya Ulaya umeanza ukurasa mpya katika historia ya kimataifa.Kile kilichoanzishwa juu juu tu na Moscow hapo 1998,sasa kinaanza kupata sura barabara.Sera za ulaya sasa zitashawishiwa kutoka dola tatu –moja ile ya wahafidhina ya Ufaransa, ile ya wajamaa wa kidemokrasi ya Ujerumani na ile ya utawala wa kimabavu ya Russia
Imedhihirika tangu kikao hiki cha Sotschi kwamba kanzela schröder wa ujerumani na rais Chirac wa Ufaransa wanaridhiana sasa moja kwa moja na tafsiri ya ugaidi alioitoa mwenzao Wladmir Putin.Kwahivyo, mkandamizo wa kikatili wa makundi ya wachache katika taifa sio unafumbiwa hapo macho bali hatua kwa hatua unaidhinishwa kimataifa."Hilo lilikua Kölnische Rundschau.
Gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE linalochapishwa Erfurt lachambua
"Mkutano huo wa kilele pamoja na Ujerumani na Ufaransa huko Tsoschi, ulienda bila mabishano na kwa urahisi kweavile ulileta maafikiano juu ya mada inayokubaliwa na wote ya kupiga vita ugaidi.
Umoja huu umeibuka kutokana na msimamo wa dola hizo 3 wa kutoafikiana na Marekani juu ya vita vya Iraq.
Kwamba wamependezewa na umoja wao huo ,imedhihirika sasa kwa kukutana tena kwa viongozi hao watatu.Kwani shinikizo kubwa kutoka kwa rais Bush kuzitaka nchi za Ulaya kuchangia zaidi katika kuijenga upya Irak baada ya vita ,ni rahisi zaidi kulikabili katika jkumu la pamoja."-laandika THÜRINGER ALLGEMEINE.
Katika gazeti la STRAUBINGER TAGEBLATT tunasoma:
"Wakiungana katika msimamo wao wa kupinga vita viliovyopaliliwa na Marekani na uingereza dhidi ya Iraq,muungano wa dola tatu umeibuka na kuimarika.Ili kujipatia rafiki katika jukwaa la kimataifa,kanzela Schröder wa Ujerumani ,amejitoa kimaso maso kwa kudai kwamba katika uchaguzi wa Chechnia,iliofanyiwa njama na hila matokeo yake na Russia,hakujazuka fujo kubwa.Nae rais wa dola kuu la Ufaransa akaitikia pia.Kanzela wa ujerumani hajakosea hapo.Kwahivyo, mualiko wa rais Putin wa Russia-mkono kwa mkono-urafiki kwa mafuta-umepokewa mikono miwili."Huo ni uchambuzi wa TAGEBLATT.
Ama gazeti la NÜRUNMBERGER ZEITUNG likitufungia mada hii laandika:
"Hapa ni swali la masilahi ya kiuchumi,la nafasi za kazi na la kupalilia kufufuka na kustawi kwa uchumi huo.Inatokana na kupanda mno kwa bei za mafuta ya petroli yanayozidi kuwa haba.Urusi ndie msafirishaji wapili mkubwa wa mafuta baada ya saudi Arabia na hivyo aweza kzisaidia nchi hizi mbili na rais Putin ameshawakubalia hayo."
Gazeti la BERLINER KURIER linachambua daraja iliofikiwa ya mageuzi humu nchini kwa jicgho hili:
"Wanasiasa kukiri makosa ni nadra.Gerhard Schröder sasa ameungama makosa.Hata chama chake cha Social Democrat kinateseka na mchango wake katika mrundiko mkubwa wa sera za mageuzi yasiopitishwa.Kwahivyo, Schröder anataka kutuarifu mambo 2:
Kwanza anajaribu kuondoa dosari.Pili,anapitisha mageuzi yaliosalia. Lakini yote anayoazimia kufanya, lazima yafanyike sasa.Ama sihivyo, itakua kaula na chua,kwa uvivu wa kuchagua.Wasocial democrat ndio wana sehemu ya jukumu la hali hii,lakini jukumu lao ni dogo.jukumu kubwa kwa hali iliofikiwa ya kuzorota kwa mageuzi linaangukia mabegani mwa Chama cha Upinzani.
Mwishoe, gazeti la ESSLINGER ZEITUNG laongeza:
"Ikiwa Ujerumani isonge mbele,lazima ijiandae kukabili changamoto za siku zijazo:Kila mmoja anapaswa kukabili changamoto hizo, nazo ni mageuzi.Lakini serikali haiwezi kuzalisha nafasi za kazi wala kustawisha uchumi kwa mazingaombo ya uchawi.Dhahiri ni kurekebisha makosa yaliofanywa tangu awali kwa kuwazindua wananachi mzigo gani wameubeba kwa kuziunganisha nchi mbili za Ujerumani-mashariki na magharibi.Dosari hiyo ndio inayoipa taabu serikali ya sasa ya muungano kati ya chama cha kijamaa wa kidemokrasi-SPD na kile cha walinzi wa mazingira cha KIJANI."