1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa Shanghai wafanyika leo India

4 Julai 2023

Iran inatarajiwa kujiunga na shirika la ushirikiano la Shanghai ambalo leo linafanya mkutano wake nchini India. Rais Vladimir Putin wa Urusi anatarajiwa kuhutubia mkutano huo wa kilele.

https://p.dw.com/p/4TNza
Russland | Videokonferenz Treffen SCO Rat
Picha: Alexander Kazakov/dpa/picture alliance

Hotuba ya Putin itakuwa ni ya kwanza katika mkutano wa kilele tangu Urusi iliposhuhudia uasi wa muda mfupi uliofanywa na kundi la mamluki la Wagner mjini Moscow.

Shirika la habari la taifa la China limeripoti kwamba rais Xi Jinping atahudhuria mkutano huo wa wanachama wanane unaofanyika kwa njia ya mtandao.

India ni mwenyekiti wa sasa wa kupokezana wa shirika hilo la ushirikiano la Shangai ambalo makao makuu yake yako Beijing.

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alisema Ijumaa kwamba,Iran itathibitishwa kuwa mwanachama kamili wa muungano huo katika mkutano wa leo,utakaoongozwa na waziri mkuu wa India Narendra Modi.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW