1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Mkutano wa kuchangisha msaada kwa Lebanon waanza Paris

24 Oktoba 2024

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amefunguwa mkutano wa kuisadia Lebanon mjini Paris, kuchangisha mamilioni ya dola pamoja na kuendeleza juhudi za kidiplomasia kutafutia ufumbuzi vita vinavyoikabili nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4mB14
Rais Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati
Ufaransa inatumai kuwa uhusiano wake wa karibu wa kihistoria na Lebanon unaweza kusaidia kuleta suluhuPicha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Ufaransa, ambayo ina mahusiano ya kihistoria na Lebanon, pia inataka kutumia mkutano huo kutafuta njia ya kuongezwa msaada wa kibinadamu nchini Lebanon.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot alikiambia kituo cha utangazaji cha RTL jana kwamba kiasi mataifa 70 na mashirika ya kimataifa 15 yanashiriki mkutano huo wa Paris, akiahidi kwamba Ufaransa haitoitupa mkono Lebanon.

Israel na Iran hazimo kwenye orodha ya mataifa yatakayoshiriki mkutano huo. Jana Rais Macron alikutana na Waziri Mkuu wa Lebanon, Najib Mikati, katika kasri la Elysee.

Ufaransa inatumai kuwa uhusiano wake wa karibu wa kihistoria na Lebanon unaweza kusaidia kuleta suluhu si tu la usitishaji wa mapigano, bali pia la muda mrefu kwenye eneo hilo.

Kabla ya mkutano huu wa kimataifa wa misaada mjini Paris, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema anataka "kutoa misaada ya kibinadamu, kuunga mkono jumuiya ya kimataifa na kuunga mkono vikosi vya jeshi la Lebanon kuimarisha usalama, hasa kusini mwa Lebanon."