Mkutano wa kukabiliana na taka za plastiki waanza Ottawa
23 Aprili 2024Matangazo
Shinikizo linaongezeka kwa wajumbe kufikia rasimu ya makubaliano kabla ya duru ya mwisho ya mazungumzo nchini Korea Kusini mwezi Disemba.
Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ziliweka shabaha ya kuafikiana juu ya mkataba wa kimataifa ifikapo mwisho wa mwaka huu. Lakini mkutano wa awali uliofanyika Kenya mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita haukupata mafanikio makubwa.
Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, tani zipatazo bilioni 9.2 za plastiki zimezalishwa tangu mwaka 1950. Idadi kubwa ya taka hizo haziwezi kuoza na hivyo kuishia kurundikana baharini na mitaani.