1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Tories na ziara ya Erdogan Magazetini

Oumilkheir Hamidou
1 Oktoba 2018

Tutamulika mkutano wa chama cha Tories cha Uingereza mjini Birmingham, ziara ya rais wa Uturuki Erdogan nchini Ujerumani na mjadala kama chama cha AfD kinaweza kuunda serikali ya muungano pamoja na vyama vikubwa."

https://p.dw.com/p/35mx6
England Parteitag der Konservativen in Birmingham Theresa May
Picha: Reuters/T. Melville

Tunaanzia Birmingham ambako waziri mkuu wa Uengereza Theresa May amepania kuona mipango yake kuelekea Brexit inaungwa mkono chamani. Gazeti la  "Mannheimer Morgen" linaandika: "Theresa May anatiwa kishindo kikubwa. Itadhihirika mjini Birmingham kama atafanikiwa kuwatuliza wanaomkosoa na kwa namna hiyo kupata uungaji mkono wa walio wengi kwa mpango wake wa kuitoa Uengereza katika Umoja wa ulaya Brexit. Ili aweze kufanikiwa anahitaji  dira ya kuaminika kwaajili ya chama chake na muhimu zaidi kwaajili ya nchi yake."

Boris Johnson ashindana na Theresa May

Gazeti la  Stuttgarter Zeitung linazungumzia mvutano kati ya Theresa May na waziri wake wa zamani wa mambo ya nchi za nje Boris Johnson. Gazeti linaandika:"Boris Johsnon hajakawia kushambulia mara baada ya mkutano mkuu kuanza. Ingawa Theresa May amejitetea, lakini bado hajatoka mashakani. Na nafasi aliyonayo ni ndogo. Pekee siku zinazokuja ndizo zitakazobainisha kama atasalimika. Dhahiri ni kwamba msimu wa mapukutiko hautasababisha majani pekee kupukutika."

Ziara ya rais wa Uturuki Ujerumani

"Ziara rasmi ya rais wa  Uturuki Recep Tayyip Erdogan imemalizika. Kilichotegemewa hakikuwa, linaandika gazeti la "Volksstimme" : "Ingawa kansela Merkel, sawa na rais wa shirikisho Frank-Walter Steinmeier na waziri mkuu wa jimbo la Northrhine Westphalia  Armin Laschet wameitumia fursa walioipata na kumuelezea rais Erdogan msimamo wao kuhusu hali ya haki za binaadam namna ilivyo nchini UIturuki, na hasa dhidi ya vizuwizi vinavyowekewa taasisi za sheria na vyombo vya habari pamoja na kushikiliwa jela wajerumani kwasababu za kisiasa. Hata hivyo yote hayo hayakusaidia kitu. Erdogan anaendelea kudai vyombo vya sheria na vyombo vya habari ni huru nchini mwake na kwamba sehemu kubwa ya waliokamatwa ni magaidi."

Eti AfD wanaweza kuunda seriokali ya muungano?

Mada yetu ya mwisho inajishughulisha na suala la wajerumani wanaotaka kujua kama kuna uwezekano wa kuundwa serikali ya muungano pamoja na chama cha AfD. Gazeti la Oberhessische Zeitung linaandika: "Wapiga kura wanataka kujua kwanini wanasiasa wa Ujerumkani wanawachukulia wafuasi wa AfD kua ni hatari kwa demokrasia. Suala hilo wanatakiwa wana CDU walijibu kwa dhati na wana SPD pia walijibu tena bila ya kinyongo."

 

Mwandishi:Hamidou Oumilkheir/Inlandspresse

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman