Mkutano wa WTO hauna dalili za makubaliano
1 Machi 2024WTO ilisema hadi siku ya Alhamis (Februari 29) hakukuwa na dalili za mwafaka kuhusiana na mazungumzo ya kuweka sheria mpya za biashara duniani.
Katika baadhi ya vikao, majadiliano yaliendekea hadi usiku wa manane, maafisa wakitafuta makubaliano katika mabadiliko kadhaa katika sheria za biashara.
Soma zaidi:Nchi zinazolima pamba Afrika zaitaka WTO kusaka suluhisho
Msemaji wa WTO, Ismaila Dieng, alisema mawaziri walikuwa wanafanya juhudi na wanapiga hatua.
Mkutano huo wa kila baada ya miaka miwili ulitaka yapatikane makubaliano ya kuondosha ruzuku za uvuvi na kuongeza muda wa malipo ya madeni katika ushuru wa biashara za kidijitali.
Afrika Kusini na India zinapinga hatua hiyo.
Tangazo la makubaliano ya mwisho liliahirishwa hadi Ijumaa (Machi 1).