SiasaChina
Mkuu wa NATO aionya China dhidi ya kuisaidia Urusi kijeshi
5 Aprili 2023Matangazo
Stoltenberg amesema baada ya mkutano na mawaziri wa mambo ya kigeni wa Muungano huo kuwa utoaji wa msaada wa silaha za kivita wa China kwa Urusi utakuwa kosa kubwa la kihistoria lenye athari makubwa.
Washirika wa NATO waliwaalika wawakilishi kutoka Australia, New Zealand, Japan na Korea Kusini kuijadili China kufuatia ziara ya Rais wa China Xi Jinping mjini Moscow.
Pamoja na msimamo wa kiuchokozi wa Beijing kuelekea Taiwan, washirika wa NATO wamejadili athari za vita vya Ukraine kwa kanda ya Indo Pacific.