Mkuu wa NATO amkingia kifua Kansela Scholz
23 Desemba 2024Matangazo
Hivi majuzi Zelensky alimkosoa Scholz kwa kitendo chake cha kuzungumza na rais wa Urusi Vladmir Putin kinyume na matakwa yake. Zelensky mara zote amekuwa akisisitiza kupatiwa makombora ya Taurus yaliyotengenezwa nchini Ujerumani na yenye uwezo wa kupiga maeneo makubwa ya Urusi. Mark Rutte amesisitiza kwamba makombora hayo yanaweza kuisaidia Ukraine katika vita vyake lakini suala hilo linabaki kuwa maamuzi ya Ujerumani kuamua kutoa vifaa hivyo vya kijeshi ama la. Scholz amekataa kutoa vifaa hivyo bila kujali maamuzi yaliyochukuliwa na washirika wenzake wa NATO akisema kwamba hatua hiyo inaweza kuleta hatari zaidi ya kutanuka kwa vita hivyo.